Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili aliojifungua Machi 28, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili juzi,
Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto
wake wa kwanza,lakini kukatokea hitilafu ndogo ya mwanaye huyo kukatwa
kidogo na mkasi uliosababisha jeraha kwenye paji la uso.
“Waliniambia walimgusa kidogo kwa
bahati mbaya na mkasi, lakini wakasema hakuna tatizo, waliniwekea
kifuani na damu ikawa imenivujia kidogo, baadaye nilijisikia uchungu
tena, manesi wakamtoa mtoto yule kifuani kwangu ili nipate nafasi ya
kujifungua tena, nilipojifungua walinionyesha motto wa kiume,” alidai
mama huyo.
Shakila alidai kuwa, tofauti na
matarajio yake, alikabidhiwa mtoto aliyejifungua wakati huo huku Yule wa
mwanzo akipewa maelezo yasiyoeleweka. “Niliwashangaa manesi.
Waliponiona sibabaiki kuhusiana na mtoto wangu ndipo wakaniletea mtoto
mwingine wakidai kuwa ndiye huyo. Nilipomchunguza nilibaini kuwa alikuwa
wa kiume wakati mimi nilimzaa wa kike, halafu huyu niliyeletewa hakuwa
na kijereha.
No comments:
Post a Comment