Jokate Mwegelo yupo single ... Staa
huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo Jumatatu hii kwenye kipindi kipya
cha TV1, ‘The One Show’ anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden
Jumanne aka The Rocker.
Katika kipindi hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza kwa
kuhojiana wao kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate ni
kama yupo kwenye uhusiano wowote wa mapenzi. Jokate ambaye pamoja na
kuwa muigizaji wa filamu pia ni muimbaji wa muziki na mjasiriamali,
alisema kuwa kwa sasa yupo single lakini haimaanishi kuwa wanaume
hawamsumbui kumtaka kimapenzi.
Jokate amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa basketball
wa timu ya Oklahoma City Thunder, Mtanzania Hasheem Thabeet pamoja na
uhusiano uliodumu kwa kipindi kifupi na staa wa muziki, Diamond
Platnumz.

No comments:
Post a Comment