MUIGIZAJI wa ‘long time’ katika
tasnia ya filamu Bongo, Brandina Chagula ‘Johari’ juzi kati amefunguka
kuwa kwa sasa hayuko na aliyekuwa akidaiwa kuwa ni mpenzi wake, Vicent
Kigosi ‘Ray’ ila yuko katika Kampuni ya RJ ambayo wanashirikiana kisanii
zaidi.
Akizungumza na Ijumaa katika
hoteli ya Johannesburg, Sinza Mori jijini Dar, Johari alisema kuwa kwa
sasa angependa atambuliwe kuwa anafanya kazi na Ray katika hiyo kampuni
na si kuhusishwa naye kimapenzi.
“Naomba ifahamike kwamba mimi niko RJ na siko na Ray kama watu wengi wanavyozungumza,” alisema Johari kwa kifupi kisha kuendelea na hamsini zake.
“Naomba ifahamike kwamba mimi niko RJ na siko na Ray kama watu wengi wanavyozungumza,” alisema Johari kwa kifupi kisha kuendelea na hamsini zake.

No comments:
Post a Comment