12 April 2014

HUU NDO UJUMBE MZITO WA HUMMER Q KWENDA KWA MR.NICE


HUMMER Q

MR.NICE
Yaani ktk watu ambao huwaonea huruma mmoja ni Nice, mda mwengine huhis kama anaonewa yaani nikupigwa daily dah , pole bhana naskia juzi walikupiga tena, ngoja nikwambie kitu kimoja bro tafuta mwanasaikolojia aweze kukusaidia kubadilisha mfumo wa maisha yako ya zamani ili uwe mpya ni wachache wanaojua maumivu yaliyomo moyoni mwako wengi wao wanakucheka wanakusema vibaya wengineo ulikula nao bhata sasa hv wamekimbia na ndio wanaokudharau kwa kupoteza pesa uliokuwa nayo mwanzo usilazimishe kwenda sehem za starehe kama huna inshu maalum hayo mambo waachie watoto we umeshafanya starehe mpaka umelamba sahani jaribu kubadilika bro kwani uswahilini kwenu hakuna vigrosary ?mbona kilevi ni kile kile bro, hebu njoo uswahilini kwetu uchukue mfano wa maisha ya kaka mkubwa jumaneture kama hana inshu ya kumpeleka sehem ya starehe basi ni story kitaa na mambo yote tunamaliza kitaa kwakuepuka mambo ya aibu kama haya unajua kuna watu wakishakujua we ni flani huwa wanatafuta chokochoko makusudi ,hizi kila Msanii anazijua mda mwengine mtu anakutukana bila sababu, au anakuzungumza vibaya kama muandishi wa historia yako kumbe hakujui hata ulipotokea ,badilika brother tafuta mwanasaikolojia atakusaidia hata Mimi nilikua na maisha ya ajabu sana ila nikaona sio maisha sahihi na sifanani na mambo ya ajabu sasa hivi najihisi mpya kabisa baada ya kukutana na wanasaikolojia ni ushauri tu bro tumetoka mbali ulinilipa elfu kumi uzinduzi wako wa kwanza kule kwetu znz kipindi kile 99/2000 kama sikosei ila we fuata huo Ushauri tu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname