Baadhi
ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti wa Bongo Movie(Steve
Nyerere) na Single Mtambalike wakiwa pembeni ya Mkurugenzi wa Msama
Promotions Limited Bw Alex Msama kwa ajili ya kumpa pole na kumfariji
mara baada ya kupata ajali wakati akitokea Dar Es Salaam kuja Dodoma,
ajali iliyotokea Ipagala Mwisho Kilometa chache tu kufika Dodoma
Mjini.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
=====
Mkurugenzi
wa Msama Promotion, Bw Alex Msama amepata ajali leo, eneo la Ipagala
mwisho wakati akitoka Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma, ajali hiyo
imemuhusisha Dereva wa Bodaboda na gari la Bw Msama kugongana, Katika
Ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Akiongea
na Mtandao wa Lukaza Blog, shuhuda ambae hakupenda jina lake kutajwa
alisema "Gari la Bwa Msama lilikua likitoka Njia ya Morogoro Dodoma
akielekea Dodoma Mjini wakati akiwa anaendesha gari, kuna bodaboda
alikuwa akitokea Mjini Dodoma mara akaingia barabarani bila kuangalia
mbele yake ndipo alipogongana na gari la Bw Msama".
Mara
baada ya ajali hiyo kutokea ,walifanikiwa kukimbizwa katika hospitali ya
Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupata Matibabu zaidi. Baada ya kufikishwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma walipokelewa vizuri na kupelekwa
chumba cha X-ray kwaajili ya kuangaliwa na mara baada ya kumalizika kwa
vipimo vya X-ray walipelekwa Wodi namba moja kwa ajili ya uangalizi wa
madaktari na manesi.
Hali
ya wagonjwa wote inaendelea kuwa nzuri mara baada ya kupatiwa matibabu
ya haraka na kupatiwa vipimo. Wagonjwa wote wamelazwa Wodi namba 1
katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment