Wananchi wakiandamana kufunga barabara ya Esso |
Askari wa jeshi la polisi tarafa ya sisimba akizongwa na waendesha bodaboda eneo la mafiati |
Barabara zimefungwa kwa kuwekwa mawe eneo la Esso |
Gari ya Polisi iliyovunjwa kioo |
Baadhi ya Bodaboda zilizoharibiwa katika vurugu hizo |
Mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya Richard Mchomvu akiwasihi vijana kuacha vurugu |
Shule ya sekondari ya Forest ya Jiji la Mbeya ililazimika kuahirisha mitihani ya kufungia mhula kutokana na wanafunzi kuathirika na mabomu yaliyokuwa yakirushwa na jeshi la polisi. |
Baadhi ya wapita njia wakiwa wameadhirika na moshi wa mabomu ya machozi |
Askari wakitoa mawe barabarani |
Baadhi ya wanaotuhumiwa kufanya vurugu wakishushwa katika kituo kikuu cha polisi |
Vurugu
kubwa zimetokea mkoani Mbeya baina ya Jeshi la Polisi na waendesha
bodaboda(pikipiki) baada ya jeshi la polisi kutaka kuzima jaribio la
kutaka kuvunja nyumba.
Boda
boda hao walifunga barabara na kuzua taflani baina yao na jeshi la
Polisi baada ya Jeshi hilo kuingilia kati kumuokoa Mke wa dereva wa
pikipiki baada ya madereva hao kuvamia nyumba yake maeneo ya Forest
wakitaka kubomoa wakimtuhumu kuhusika na kifo cha mumewe.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya saa nne asubuhi baada ya waendesha
bodaboda kutaka kumdhuru mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua dereva
mwenzao ndipo jeshi la polisi lilipoingilia kati hivyo kusababisha
vurugu kubwa baina ya madereva hao na jeshi la polisi.
Hata
hivyo madereva wa pikipiki zaidi ya 20 walilivamia gari la Polisi na
kuvunja kioo cha mbele hali iliyopelekea dereva wa gari hilo
kulikimbiza hadi kituo cha Polisi cha Kati ili kuomba msaada kwa askari
wenzie waliojitokeza wakiwa na silaha za moto na kuwatawanya kabla ya
kufunga barabara na kuanzisha vurugu.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waendesha bodaboda Jiji la Mbeya, Vicent Mwashoma,
amelaani kitendo hicho na kuongeza kuwa jeshi la polisi limetumia nguvu
kubwa kupambana na madereva wa bodaboda ili hali kuna uongozi
unaotambuliwa na kusimamiwa na baadhi ya Askari.
Akizungumzia
chanzo cha vurugu hizo, mwenyekiti huyo amesema juzi aliuawa dereva
mwenzao aliyemtaja kwa jina la Siza Mwambenja ambapo baada ya kuzika
madereva hao walianza kufanya upelelezi na kupewa taarifa kuwa
aliyehusika ni mkewe aliyeachana naye kwa kusuka njama na wauaji.
Amesema
baada ya kupata taarifa hiyo walienda nyumbani kwake kwa lengo la
kumkamata hali iliyosababisha jeshi la polisi kufika na kuwatawanya
lakini jazba ziliwapanda madereva hao baada ya baadhi ya maaskari kuanza
kuvunja pikipiki na kuwapiga.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha mauaji hayo ni
wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuachana na mke wake huyo
anayetuhumiwa kusuka njama za mauaji na kuoa mke mwingine hali
iliyosababisha mwanamke huyo kupata wivu na kulazimika kufanya mipango
ya mauaji hayo.
Wakati
vurugu hizo zikiendelea Shule ya sekondari ya Forest ya Jiji la Mbeya
ililazimika kuahirisha mitihani ya kufungia mhula kutokana na wanafunzi
kuathirika na mabomu yaliyokuwa yakirushwa na jeshi la polisi.
Hata
hivyo kufuatia vurugu hizo waendesha boda boda kadhaa wanashikiliwa na
jeshi la polisi akiwemo Katibu wa chama hicho kwa kuhusika na uvunjaji
wa Sheria na uharibifu wa miundombinu ya barabara na gari la Polisi.
Via > Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment