
E LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya
kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.


Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.

Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”
No comments:
Post a Comment