Mama
mmoja maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara
King’ongo jijini Dar es Salaam aliyenaswa kwa kosa la kumtumikisha
mwanaye wa miaka 13 kazi nzito.
MAMA mmoja
maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara King’ongo
jijini Dar es Salaam amenaswa kwa kosa la kumfanyisha mwanaye kazi nzito
zisizoendana na umri wake wa miaka 13 (picha ndogo). Majirani
wa mama huyo walitoa taarifa kwa waandishi wetu wakidai kuwa, mwanamke
huyo humfanyisha kazi nzito mtoto wake huyo kama mfanyakazi wa ndani
akiwatunza wadogo zake huku akiuza genge lililopo karibu na nyumbani
kwao.
Mtoto Saumu Shaban (13).
Ilidaiwa
kuwa pamoja na kazi hizo ngumu, mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina
la Saumu Shaban (13) hukaanga chipsi kuanzia mishale ya jioni mpaka
usiku wa saa 5 ambapo hufunga shughuli zake kabla ya siku inayofuata
kurudia utaratibu huo.
No comments:
Post a Comment