01 April 2014

ANGALIA PICHA KIJANA AUAWA BAADA YA KUIBA PIKIPIKI

Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia leo katika mtaa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar ziliibiwa.Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai wanatafuta pikipiki iliyopotea.
Mashalia ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.
Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.
KIJANA ALIYEUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO 
BOFYA HAPA KUANGALIA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname