04 April 2014

ANGALIA NAFASI MPYA ZA KAZI KUTOKA UTUMISHI LEO

MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II)

MCHUMI DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 23)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango na Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia .
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhudumia kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati ya mahesabu ya mashirika ya Umma)
 Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
 Kufanya utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
 Kufanya utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
 Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi namaendeleo ya jamii.
 Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo;
 Uchumi (Economics)
 Takwimu (Statistics )
 Sayansi ya Uchumi Kilimo (BSc Agriculture Economics & Agribusness) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname