01 April 2014

ANGALIA MATESO:UGONJWA WA JICHO UNAOMSUMBUA MTOTO AMBALO LIMEFUMUKA NA KUTOKA NJE

Mtoto Neema Joseph (2) akilia kutokana na maumivu makali ya jicho.
KWELI ni zaidi ya mateso! Ukisema we unaumwa lakini unapata usingizi, kumbe hujawaona wagonjwa wenyewe!  Mtoto Neema Joseph (2) anateseka kwa ugonjwa wa jicho ambalo limefumuka na kutoka nje huku likitoa harufu kali na maumivu yasiyo na mfano,Mtoto huyo anayelia wakati wote kutokana na maumivu, anaishi na mama yake mzazi, Annastazia Yohana (28) kwenye Kijiji cha Bugomba, Kata ya Bulungwa wilayani Kahama, Shinyanga.Akizungumza huku akimwaga machozi kwa uzito wa tatizo la mwanaye, mama Neema alisema hali yake ya  maisha kiuchumi ni mbaya, hasa kufuatia kufiwa na mumewe, Josephat miezi tisa baada ya kujifungua mtoto huyo huku akiwa analea watoto wenginewawili.
SIKIA KILIO CHA MAMA NEEMA
“Tangu mume wangu afariki dunia nimekuwa na maisha ya shida, sina msaada kwani hakuna ndugu wa mume wala wangu wenye hali nzuri ya maisha na walio tayari kunisaidia kubeba mzigo wa maisha yangu.ANGALIA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname