AJALI...AJALI....AJALI...DEREVA WA BASI LA PRINCES MURO MATATANI KUUA KWA KUGONGA MTEMBEA KWA MIGUU IRINGA
NA
FRANK KIBIKI JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva wa basi
la abiria la PrinceS Muro, ambalo hufanya safari zake kati ya Mbeya na
Dar es salaam, Said Mtatifikolo, kwa tuhuma za kumuua mtembea kwa miguu
baada ya kumgonga. Kaimu Kamanda wa jeshi hilo, Nyingesa alisema kuwa
ajali hiyo, imetokea juzi jioni katika eneo la Viwengi wilayani Iringa.
Nyigesa alisema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo lenye namba za
usajili T 528 BVP, kumgonga na kumuua mtembea kwa miguu ambaye jina lake
bado halijafahamika kutokana na mwili wake kuharibika. Hata hivyo
alidai kuwa upelelezi juu ya ajali hiyo unaendelea na kwamba, mtuhumiwa
huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika.
No comments:
Post a Comment