Makubwa! Kichwa cha Bongo Fleva kutoka
pande za Kimanzichana mkoani Pwani, Abas Kinzasa ‘20%’, anadaiwa kunaswa
laivu akiwa kwa mganga wa kienyeji akipata tiba ya kupunguza na kuondoa
sumu ya utumiaji wa bangi na pombe, Ijumaa Wikienda lina ‘pakeji’
kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, ishu
hiyo ilijiri katika Kijiji cha Ngukumo mkoani Tabora baada ya mameneja
wa wasanii wa Bongo Fleva, Papa Misifa na Steve Mbaga kumshika mkono 20%
na kutafuta mganga wa kienyeji ambaye aliwatangazia kuwa ana dawa
zinazoweza kumuondoa sumu hiyo.
Baada ya kunyetishiwa stori hiyo, gazeti
hili liliwatafuta mameneja hao ambao walisema walilazimika kufanya
hivyo ili waweze kumrudisha 20% kwenye gemu kwa mara nyingine kwani bado
wanaamini ana uwezo mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.
“Kiukweli mimi na mwenzangu tumekuwa
tukisikitishwa kwa muda mrefu baada ya 20% kubobea kwenye matumizi ya
pombe na bangi na hasa alipozidiwa hadi akashindwa kufanya muziki huu
ambao tunaamini kwake ndiyo ilikuwa ajira pekee.
“Kwa kutambua hilo tulimtafuta na
kuongea naye, alipokubaliana nasi tukaamua kumpeleka kwa mganga wa
kienyeji, ameshapata tiba na tayari ameonyesha kujitambua, hivyo hivi
karibuni tunaanza kufanya naye kazi na ndiyo tunatoka kumlipia nyumba ya
kuishi maeneo ya Mwananyamala Hospitali,” alisema Papa Misifa.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta 20% ambaye
mwaka 2011 alichukua tuzo tano za Kili na kumuuliza juu ya suala hilo
ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Papa Misifa na Steve Mbaga
wamejitahidi sana kunifanya niachane kabisa na matumizi ya pombe maana
walinipeleka kwa mganga wao ambaye kweli amenisaidia.
“Ujue kilichokuwa kikiniyumbisha siku
zote hizo ilikuwa ni pombe maana bangi ilikuwa si kiivyo, nilipokuwa
nakunywa pombe kweli ilikuwa ikinitoa kwenye njia na kunifanya kujiona
mimi ndiyo mimi kiasi cha kushindwa hata kuwaheshimu wenzangu na ndiyo
jambo pekee ninaloweza kusema limenifanya kuwa hivi.”
-GPL

No comments:
Post a Comment