Ni vigumu kueleza
matukio yote yaliyotawala kauli na hisia za wengi kwa wiki nzima mjini
Dodoma bila kuangalia michango ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Michango hiyo ya
mawazo katika mjadala kuhusu rasimu ya kanuni zinazopaswa kuongoza kikao
kwa siku 70 za kikao hicho, baadhi yake zilikuwa kali.
Zifuatazo ni baadhi ya kauli hizo:
Mtikila, ambaye ni
mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alitumia dakika tano kutoa somo kwa
wajumbe wa Bunge hilo kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya siri badala ya
ile ya wazi.
Anasema haki ya
kupiga kura kwa siri haitofautiani na haki ya mtu kuwa na miguu miwili
na kwamba itashangaza akitokea mtawala akaamuru kila mtu awe na mguu
mmoja, halafu watu wakakaa kujadili.
Alisema Bunge
Maalumu la Katiba litaingia katika hatia na aibu kwa kujadili mambo ya
msingi ya kidemokrasia ambayo pia yameainishwa katika katiba ya sasa,
likiwamo suala hilo la kura ya siri.
“Mwenyekiti
(akimlenga Pandu Ameir Kificho) tumekuchagua kwa kura ya siri siyo
kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni ‘democratic civility’
(ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
“Ni aibu
waheshimiwa na hii nasema si jambo la mjadala kuna vitu vya kujadili,
lakini si haki ya kupiga kura kwa siri. Hii ni haki ya msingi ya
kidemokrasia,” alisema.
2. Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti –CUF Taifa)
Mwenyekiti huyo wa
CUF alisema msingi wa kupiga kura ya siri ni kujaribu kuwalinda wajumbe
ambao wanaweza kupiga kura kinyume na misimamo ya vyama vyao au makundi
yao.
Akijenga msingi
wa hoja yake, Profesa Lipumba alisema hata Jaji Joseph Warioba katika
taarifa yake alisema moja ya taasisi zilizotoa maoni ni Baraza la
Wawakilishi lililopendekeza Serikali tatu.
“Tunadai kura za
siri kusudi kuwalinda hawa wenzetu ambao wametoa misimamo, wakija
kupiga kura hapa inaweza kuwapa matatizo huko walikotoka,” alisema.
Aliongeza :
“Tunapolishabikia hili kuwa pasiwe na kura ya siri inaonekana wazi pana
ajenda ya kuwashughulikia watakaokwenda kinyume cha msimamo.”
3. Esther Bulaya (Viti Maalumu-CCM)
Bulaya, tofuti na
wajumbe wenzake wengi kutoka chama tawala (CCM), alionekana kutoa
mchango uliogusa hisia za wengi hasa pale alipoeleza bayana kuwa hayuko
tayari kuona ukandamizaji unafanyika kumlazimisha apige kura ya wazi.
Akirejea msimamo wa kura ya wazi unaoshabikiwa na wajumbe wengi
wanaotokana na chama chake, alisema hawezi kupiga kura ya aina hiyo
wakati anajua inamnyima uhuru wake.
“Nitasema kweli
daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi katika uamuzi mgumu kama huu
kulifanyika kura za wazi kama wengi wanavyotaka,” alisema.
4. Pandu Ameir Kificho (Mwenyekiti wa Muda)
Naye Kificho,
ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, alionyesha
kukerwa na baadhi ya vyombo vya habari hasa vilipolishikia bango suala
la posho.
“Kusema kweli,
jamii tunaichanganya mpaka jambo hili la kutupatia Katiba Mpya
lionekane ni la mchezo au tumekuja kudai posho. Nawataka wenzetu
(wanahabari) wawe makini sana juu ya jambo hili wasiupotoshe umma ili
kazi hii isiingie dosari,” alisema.
“Vyombo vyote
vya habari vizingatie kupata habari kwa uwazi na ukweli kutoka kwa
wanaohusika ili jamii yetu ya Watanzania ipate habari za kweli na hilo
la kupokea tu posho kwa kusoma magazeti tunalikanusha kwa nguvu zote”.
Ndesamburo
aliwataka wajumbe wenzake kuacha ushabiki wa kisiasa na kutambua
wanatengeneza katiba itakayodumu miaka 50 ama miaka 10 ijayo.
“Tusilete
ushabiki. Nawaombeni sana tusilete ushabiki katika jambo hili. Hili ni
jambo zito. Hili ni jambo tunalolifanya kwa niaba ya Watanzania milioni
45 na sisi tumepata bahati tu; ni Mungu ametusaidia,” alisema.
6. Profesa Jumanne Maghembe (Waziri wa Maji)
Profesa Maghembe
alifananisha upigaji wa kura kwa siri kuwa sawa na ule uliofanyika
nchini Marekani wakati wa kashfa ya ufuska iliyokuwa ikimkabili
aliyekuwa rais wakati huo, Bill Clinton.
“Kule Marekani
walikuwa wakipiga kura ya kumwondoa madarakani Clinton kwa madai ya
kushikwa ugoni. Walipiga kura ya wazi kwa sababu lilikuwa jambo kubwa la
kumwondoa mtu madarakani,” alisema.
Profesa Maghembe,
ambaye pia ni Waziri wa Maji, aliwasihi wajumbe kutofautisha upigaji
kura wa mwenyekiti wa kijiji, diwani, mbunge na rais ambao alisema
wananchi hupiga kura za siri.
“Humu ndani
tunatafuta sheria mama ya nchi. Tumepewa jukumu hilo kwa niaba ya
Watanzania wote. Wao watapata nafasi ya kusema ndiyo au hapana. Sasa
tunajificha ili iweje, tunamficha nani?” alihoji.
7. Sheikh Hemed Jengo
Sheikh Jongo
alishauri Bunge Maalumu la Katiba kuwapa nafasi wajumbe wanawake
watakaokuwa katika hedhi, waruhusiwe kuapa bila kushika kitabu kitukufu,
Quran.
“Siku nyingine
kinamama wanakuwa katika siku maalumu (hedhi). Ni haramu kwa mujibu wa
dini kushika msahafu. Atakapojieleza kuwa hali yangu si nzuri, basi
aruhusiwe kuapa hivyo hivyo kwa heshima,” alisema na kuongeza:
“Hata kwa wanaume
wa Kiislaamu wakitaka kuapa wachukue udhu kwa sababu kitabu chenyewe
kinakataza kukishika bila ya udhu. Ndiyo yamini. Ndiyo maana watu
wengine hatuoni wanafanya vizuri kule nje kwa sababu wanajua waliapa
bila udhu na haikuwa yamini.”
8. Maria Sarungi Tshehai
Mwanaharakati huyo
alitumia fursa aliyopewa kuwaponda wajumbe wenzake waliokwenda katika
Bunge hilo kwa ajili ya kuwasilisha masilahi ya vyama.
“Hatuko hapa kwa ajili ya kuwasilisha vikundi mbalimbali. Tukianza hivyo itakuwa ni hatari sana katika Bunge hili,” alisema.
“Nianze kwamba kitu
kilichonifanya nitoke nje nilifutwa (na mtu ambaye hakumtaja jina).
Aliniambia wewe mbona unaonekana upo kwenye upande wa chama fulani.”
9.Richard Ndassa (Mbunge wa Sumve)
Yeye alionekana
kukerwa na baadhi ya taarifa za vyombo vya habari kuhusu suala la posho
na kuvishtaki vyombo hivyo kwa mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu
Ameir Kificho.
“Wabunge
wanachota milioni 129 kwa kikao cha dakika 30” na kingine kikisomeka,
“Wabunge walipwa milioni 130 kwa dakika 25; Bunge la Katiba vipande
vipande; wapewa posho kwa kusoma magazeti,” alisema akikariri vichwa vya
habari vya baadhi ya magazeti na kudai vinamkera.
10. Dk. Zainab Gama
Naye mwanasiasa
mkongwe, Dk. Zainabu Gama alikwenda mbali na kudai kuwa baadhi ya
wanaotaka kura ya siri wametumwa na watu ama wamekula rushwa ndiyo maana
hawataki kupiga kura ya wazi.
“Hatukuletwa hapa kimchezo mchezo. Simama, sema mimi uamuzi wangu huu kila mmoja akuone,” alisema.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment