24 March 2014

ANGALIA VIDEO YA WIMBO MPYA WA CHUNA BUZI YA SHILOLE

Usiku wa kuamkia leo director mwenye kawaida ya kutoa video zake siku inapobadilika yaani saa sita usiku, Nisher Bybee kutoka Arusha ametoa kazi yake mpya ikiwa ni ya tatu kwa mwaka huu 2014, ambayo ni video ya Shilole ‘Chuna Buzi’.Video hiyo ambayo mwanzoni inaanza na onyo la ‘Parental Avasory Explicit Content’ ikimaanisha ndani ina maudhui ambayo yanaweza kuwa hayafai kuonwa na watu fulani mfano watoto, imeonekana kuwapa wasiwasi baadhi ya mashabiki wa kazi za Nisher katika ukurasa wake wa facebook pamoja na Instagram.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname