Hapa akitia huruma
Yule
mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae
amekamtwa kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari
za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni
Raia wa South Africa aliyeahamika kwa jina la JAN ELOFF oambae anaishi
maeneo ya Msasani Jijini Dar.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na
mtandao huu hatari kwa habari za uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae
alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi
mwandamizi wa blog hiyo na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari
mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu
hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na
Kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi
la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae
alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni araia wa Cameroon na
Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukatwa
mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja
wenzake anaoshirikiana nao
Kufuatia kukamatwa kwa mzungu huyo wananchi
wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haaka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo....
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haaka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo....
No comments:
Post a Comment