05 February 2014

NATAKA KUJITOA KWENYE KANISA LA KUSALI UCHI..

Naitwa  Dada  Tunu, ni  mwanamke  mwenye  umri  wa  miaka  33,nipo  kwenye  wakati mgumu  sana  katika  maisha  yangu, najitokeza   kwenu  watanzania  wenzangu  ili mnishauri  nifanye  nini. Kwa  ufupi  ni  kwamba, niliolewa  mwaka  2001,kisha  mimi na mume  wangu  tukahamia  Morogoro. Sikubahatika  kupata  mtoto   hadi  mwaka 2010  ambapo  nilijifungua  mtoto  wa  kike, hata  hivyo  mtoto  huyo  hakuwa  riziki kwani   miaka  miwili  baadaye  alifariki  dunia, hii  ilikuwa  mwezi  Machi  2012, niliumizwa  sana  na  kifo  hicho, ukichukulia  manyanyaso  niliyokuwa  nayapata  kwa mawifi zangu, wakwe  zangu  na  mume  wangu  mwenyewe  kutokana  na  kutobeba ujauzito, miezi  mitatu  baadaye  mume  wangu  alinifukuza  na  kuoa  mwanamke mwingine.  Siwezi  kuelezea  uchungu  nilioupata. Nilifukuzwa  kama  mbwa. Nilifikia hatua  ya  kutamani  hata  kujiua lakini 
Mungu  aliniepusha. Baada  ya  tukio  hili niliamua  kurudi  nyumbani  kwa  wazazi  wangu. Nikiwa nimesharudi   nyumbani kwetu, siku  moja   nilikutana  na  dada  mmoja  ambaye  alikuwa  rafiki  yangu  wa tangu  utotoni, huyu  na  yeye  alikuwa  ameolewa  na  kuachika  kwa  mumewe, aliachwa  na  watoto  watatu, wa  kwanza  alikuwa  na  miaka  7. Nilishangaa  kumuona rafiki  yangu  huyu  akiwa  na  mafanikio  makubwa  sana. Alikuwa  na  majumba, magari na  biashara  mbalimbali . Nilijiuliza  maswali mengi  sana, kuhusu  mahali  alipo upata utajiri  wake  kwani  nakumbuka  ni  miaka  miwili  tu  iliyokuwa  imepita  nilipokuwa nimerudi  kutembea  nyumbani  nilikutana  naye  akiwa  na  maisha  magumu  sana, alikuwa  ndio  ametoka  kuachwa  na  mume  wake . Baada  ya kuongea  naye  kwa kirefu  nikimuomba  anisaidie  na  mimi  niwe  kama  yeye, aliamua  kunipeleka  kwenye kikundi  chao. Kikundi  hiki ni  cha  wanawake  walio  achwa  na  waume  zao. Dada huyu  aliniunganisha  kwa  mkuu  wa  hicho kikundi  ambaye  wao  walikuwa wanaumita  DADA  MKUBWA  ama  BIG SISTER.  Dada  mkubwa  alinihoji  maswali mengi  sana, baadaye  akaniambia  nirejee  baada  ya  siku  saba, baada  ya  siku  saba, akakichukua  na kunipeleka   kwenye  hoteli  moja  ya  kifahari  hapa hapa  jijini  Dar  Es salaam. Huko   nilikutanishwa  na  wanawake   wenzangu  kama  kumi  na  mbili  ambao nao  walikuwa  wamepelekwa  kwa  mara  ya  kwanza. Baada  ya  kupewa  maelekezo, tulipelekwa  kwenye  chumba  maalumu  ambapo  tulinganishwa  na  wanawake wengine   kama  thelathini  ambao  ni  matajiri  sana, baadhi  yao  niliwatambua  kwa sura kutokana  na  umaarufu  wao. Wengine  ni  wake  za  watu, watu  maarufu, wanafunzi  wa  vyuo  na  sekondari na  wengine  ni  raia  wa  nchi nyingine  kama  vile Nigeria, Ghana  na  Kenya.  Wote  hawa walikuwa  wamevaa  mavazi  maalumu. Tulipewa  maelekezo  maalumu  ambapo baadaye  wote tulitakiwa  kuvua nguo  zetu  na kubaki  kama  tulivyo zaliwa. Ibada  ilio ongozwa na  wanaume  watatu walio  valia mavazi  maalumu, kiongozi  wa ibada  alikuwa  mwanaume kijana  mdogo  tu  ambaye wakati  wote  alikuwa  anazungumza  maneno   nisiyo  yaelewa. Baada  ya  hapo  ikawa kila  wiki  tunarudi  tena  kufanya  ibada  hii  na  kila  wiki  kulikuwa  na  wanawake wapya  zaidi  ya  ishirini  ambao  wameletwa  kujiunga. Hapa  ndio  nikawa  nimeingia rasmi  kwenye  kanisa  hili  la  kusali  uchi  bila  kutarajia  Miezi  sita  baadaye  nikawa tayari  namiliki  nyumba  kadhaa, magari  na  biashara  zinazo  nilipa  sana. Ingawa katika  kanisa  hili  hakuna  masharti  ya  kutoa  damu  za  watu, lakini   ukiingia  katika kanisa  hili  unafanya  mkataba  maalumu  na  shetani, kwanza  utatakiwa  kumtumikia shetani  katika  maisha  yako  yote  ya  hapa  duniani  ambayo  maana  yake  ni  kwamba, unakuwa  umekubali  kuwa  na  maisha  mazuri  hapa  duniani  na  utakapo  kufa  uende jehanamu. Utapata  kila  kitu  unacho  kitu unacho  kitaka, kuanzia, pesa, magari,majumba,mapenzi, nguvu, exposure  na  kila  kitu  kizuri  unacho  kijua  wewe, lakini  kwa sharti  la  kuuza  roho  yako  kwa  shetani. Ukiingia  kwenye  kanisa  hili  ni hakuna  kutoka, wala  kutoa  siri  zao.  Ukitoka  utapata  matatizo  makubwa  na  ukijitoa ndio  balaa.  Mimi  nimeamua  kujitoa  mhanga  ili  kuwasaidia  watanzania  wenzangu hasa  wanawake  kwa  sababu  kuna  wanawake  wengi  sana  kuanzia  wanafunzi  wa shule za  sekondari, vyuo, wake  za  watu , wafanyakazi ,wafanyabiashara  hadi  watu maarufu  wamekuwa  wakijiunga  na  kanisa  hili  kila  kukicha  kwa  ajili  ya   kupata huo  utajiri wa  kishetani. Sikushauri  ufanye  hivyo  kwani  mwisho wa  siku nafsi yako itaangamia.  Binafsi  ninaumia  sana  moyoni  kuona  kuwa  nina  mali, na  utajiri mkubwa  lakini  nimeupata  kwa  shetani  na  siku  nitakayo  kufa  ninakwenda Jehanamu. Sina  raha  na  utajiri  wangu  na  ninatamani  niyatelekeze  majumba  yangu, kisha niende  nikaishi  maisha  yangu  ya  awali, ya  kimasikini  lakini  nikiwa  na  amani moyoni, ila  ninashindwa  kwa  sababu  nilisha  jifunga  na  kanisa  hili.

Ninaomba  ushauri  wenu  watanzania  wenzangu, ninataka  kujitoa  lakini  ninaogopa madhara  ninayo weza  kuyapata  kutokana  na  kujitoa. Nifanye  nini  ili niweze  kujitoa. . Unaweza  kuniandikia  kupitia  barua  pepe  yangu :  tunukondo@gmail.com

1 comment:

  1. Tueleze vizuri ukiingia hapo au ulipoingia hapo utajiri ulikujeje?Je, ulipewa magari na mapesa na hayo majumba ukaanza kuyamiliki?Huyo shetani mnaongea naye wapi na kivipi kama siyo watu wenyewe au kuna kitu kingine mnafanyiwa hujatueleza?Hao wanaume wanaoongoza ibada za kishetani huwaambia nini hasa.Na uchi wenu huo mnaowaonyesha kwenye ibada hizo wanaufanyia nini hao wanaume watatu wanaoongoza ibada zenu?

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname