Ujio wa mitandao ya kijamii kama
Facebook na Twitter umerahisisha mawasiliano kwa kiasi kikubwa.
Imerahisisha mawasiliano kati ya wasanii na mashabiki wao au wasanii na
vyombo vya habari.
Sentensi fupi kama ‘September 29 ni siku yangu muhimu, ntazindua album yangu mpya, naombeni support yenu’ kwenye
Facebook au Twitter inaweza kusafiri mamilioni ya maili na kuwafikia
mashabiki wako wengi duniani kote na vyombo vya habari vikapata habari.
Bahati mbaya ni kwamba kuna wasanii wengi wenye allergy na mitandao ya
kijamii.
Haijulikani wako wapi, wanafanya nini,
wanatoa lini wimbo mpya na kwa ufupi ni kwamba wamejichimbia shimoni.
Kama haupo Facebook, Instagram wala Twitter, unategemea jina lako
liongelewe wapi?
2.Kuanika kila kitu kwenye mitandao ya kijamii
Hakuna haja ya kuandika kwenye Twitter
au Facebook kuhusu promoter wa Kahama aliyeshindwa kukulipa hela yako ya
show na ukakosa nauli ya kurudi Dar es Salaam. Haikusaidii chochote
zaidi ya kukushusha. Blogs zitasherehekea kwakuwa zitakuwa zimepata
habari nzuri ya kuvuta traffic na kukuchoresha zaidi wewe kwa vichwa vya
habari kama ‘Ugolo Mweupe akosa nauli ya kurudi Dar baada ya promoter kumwacha kwenye mataa’.
Wewe ni staa. Unaishi ndoto. Itunze
ndoto hiyo. Usimwambie kila mtu jinsi ulivyopigika na kwamba bado
unaishi na mama yako ama kitu chochote kinachoweza kuharibu heshima kwa
mashabiki wako. Kumbuka hauuzi tu muziki wako bali pia unauza wajihi
wako.
3. Kupenda kuponda wasanii wenzako, vyombo vya habari ama wadau wengine hadharani
Kuna wasanii wanaojiona wao ndio kila
kitu. Wao ndio rappers ama waimbaji bora tangu ulimwengu uanze. Mara
nyingi tumesikia wasanii wakihojiwa redioni na kuanza kuponda nyimbo za
watu wengine kana kwamba nyimbo zao zimetungwa kwa msaada wa malaika.
Japokuwa una haki ya kutoa maoni yako pia unapaswa kukumbuka kuwa suala
la kukosoa nyimbo hadharani ni kazi ya wachambuzi wasiofungamana na
upande wowote. Unapokosa wimbo wa mwenzio na kumuita wack mcee, tambua
kuwa kuna mashabiki wengi wanaoumpenda na kwa namna yoyote utakuwa
umewakera pia.
Nakumbuka niliwahi kusikia interview ya
Hammer Q kwenye kipindi cha Leo Tena Clouds FM na kumsikia jinsi
alivyokuwa akiwadhalilisha madj wa redio zingine kuwa wanaendekeza
rushwa. Japokuwa suala hilo kweli lipo, lakini hakupaswa kuzungumza
hivyo kwenye radio inayosikilizwa nchi nzima. Nina uhakika siku hiyo
alizungumza ujumbe uliowakera watu wa radio zingine nyingi ambao kuanzia
siku hiyo walimuona snitch.
4. Kutokuwa rafiki wa vyombo vya habari
Ni ngumu kuwa karibu na redio, TV,
magazeti ama blogs zote nchini lakini ni muhimu kuziheshimu zote.
Ukiombwa interview na kituo cha radio cha Ludewa, unapaswa kuwa na
muitikio sawa na kama unapoombwa interview na radio kubwa ya Dar es
Salaam. Unapokuwa msanii mkubwa, tambua kuwa kila kona ya nchi kuna
mashabiki wako, hivyo usiwanyime fursa mashabiki wako wa vijijini kujua
habari zako.
5. Kuachia nyimbo kwa mfumo wa Exclusive
Niliwahi kuandika mada hii kwa urefu zaidi hapa.
Lakini ninao mfano halisi wa msanii mkubwa aliyeniambia kuwa kipo kituo
kikubwa kimoja cha redio ambacho hakipigi tena nyimbo zake kwasababu
alichagua kwenda kuutambulisha wimbo wake exclusive kwenye kituo kingine
cha redio.
6. Kuwa mikononi mwa meneja asiyekijua kiwanda cha muziki
Asilima kubwa ya wasanii, hasa wachanga
wapo chini ya mameneja wenye pesa lakini wasio na ufahamu wa namna
muziki wa Tanzania ulivyo. Wengi humsaidia msanii kwa kipindi fulani
akitegemea matunda yaanze kuonekana ndani ya miezi mitatu.
Kwa mazingira ya muziki ulivyo Tanzania
ni ndoto kupata mafanikio katika kipindi hicho. Ni bora kuwa na meneja
mwenye kipato cha kawaida lakini anayezijua njia na fitina za muziki wa
Tanzania, kuliko kuwa na meneja mwenye hela lakini anayeishi kwenye
ulimwengu tofauti na ule wa muziki.
7. Kufulululiza kutoa nyimbo zinazofanana
Kuna kichaa mmoja alipita sehemu na
kuokota noti ya shilingi elfu moja. Basi kuanzia siku hiyo, alihakikisha
anapita eneo hilo zaidi ya mara 20 akitegemea kuwa ataokota tena hela
nyingine. Huo ni mfano wa namna baadhi ya wasanii wa Tanzania walivyo.
Wimbo mmoja ukiwa hit, basi atahakikisha zingine mbili mpya zitakuwa ama
na beat inayofanana na ya mwanzo ama ujumbe/mashairi sawa na wa mwanzo.
Kwa mfumo huo, ni ndoto kufululiza kutoa hits bali utakuwa kama
unaachia series au remix za nyimbo zako.
8. Kutokuwa na producer mmoja anayekupatia
Simaanishi kuwa kila msanii awe na
producer mmoja tu wa nyimbo zake. Maana yangu ni kwamba, kuna namna
ambavyo inatokea producer mmoja humpatia zaidi msanii fulani.
Kwa Tanzania tunafahamu jinsi Mika
Mwamba anavyompatia Mad Ice, Mona G anavyowapatia Young Killa na Belle
9, marehemu Roy alivyokuwa akiwapatia Mr Blue na Abby Skillz, KGT
anavyompatia Ali Kiba, John Mahundi anavyompatia Crazy GK, P-Funk
alivyompatia Jay Mo, Juma Nature na wengine.
Mfano wa Marekani, Timbaland
anavyompatia Justin Timberlake, 40, Matthew Jehu Samuels Boi-1da na
T-Minus wanavyompatia Drake, vocals zote za nyimbo za Rihanna hufanyiwa
kazi (produced) na Makeba Riddick aka Girl Wonder, nyimbo karibu zote za
Jay-Z lazima zipitie mikono ya Rick Rubin na wengine.
9. Kutafuta Kiki
Kila mmoja anapenda kupata Kiki lakini
wakati mwingine Kiki zimewatokea puani wasanii wengi. Tafuta kile
ninachoweza kukiita ‘Intelligent Kick’ na sio ‘Mediocre Kick’.
10. Timing ya kuachia wimbo
Unapofikiria muda wa kuachia wimbo
inabidi utulize akili kidogo sababu unaweza kujikuta ukitupa jiwe
gizani. Angalia muda mzuri wa kuachia wimbo usije ukaachia katika muda
ambao wimbo wake utapotea kwenye rotation baada ya wiki moja tu.
11.Kutojipigia debe
Hivi karibuni nilipiga story na rapper
Wakazi na akanieleza jinsi anavyofanya mambo yake. Kwa kiasi kikubwa
jina lake limefahamika kwa jitihada zake mwenyewe na tena kwa promotion
ya online. Alikuwa akihangaika mwenyewe kujipigia promo kupitia mitandao
ya kijamii na kushirikisha blog zingine. Baada ya kuona watu wengine wa
blog wanambania, akafungua blog yake mwenyewe kibishi na kuandika issue
zake. Ukiwa mmoja wa followers wake, unaweza kugundua kirahisi jinsi
anavyojipromote mwenyewe kwa kuandika tweets kama; Pls Request “Touch”
by Wakazi on your favorite radio station.
Usipojipromote mwenyewe, ni nani mwingine atafanya hivyo?
Usipojipromote mwenyewe, ni nani mwingine atafanya hivyo?
12. Kulazimisha kushawishi watu wasikie/wacheze wimbo wako
Haina haja ya kulazimisha watu kwa
kuwatag Facebook wasikilize nyimbo zako online. Mara nyingi ukiwa msanii
msumbufu wa kuwapigia simu watangazaji kila siku na meseji zisizo na
kichwa wala miguu, unajiweka cheap na kujishusha.
Kama mtangazaji hajaupenda wimbo wako
kwakuwa ni kweli si mzuri, usijaribu kumshawishi kwasababu, kama ni
mbovu hatoucheza. Na kadri unavyoendelea kumsumbua acheze wimbo wako,
ndivyo anavyokumbuka jinsi ulivyogeuka kero kwake.
Hiyo ina maana kuwa utajiharibia hata kwenye ngoma zako zijazo.
13. Kushindwa kutengeneza uhusiano mzuri na mashabiki wako
Hakuna mtaji mkubwa kama mashabiki. Kama
utakuwa na uhusiano nao mzuri, hawatakuangusha kamwe. Watu si wajinga.
Wanafahamu sana pindi unapotaka wanunue ama wasikilize kazi zako. Kama
una uhusiano mzuri na mashabiki wako na wanajua unawajali watakusupport
kwa kila kitu.
Kwenye makala yake aliyoipa jina; ‘6 lessons artists must learn from ‘anacondagate’ Mwandishi na gwiji wa masuala ya Masoko, Constantine Magavilla aliandika:
Loyal fans outstrip money in the long
run so never undermine them. They will come out and support you when you
need them most! The worst thing you can do is not to appreciate your
fans when you are on top of the world. Remember, your social
significance and earnings are a function of the number fans you have and
the value each brings to the table.”
Kila siku – haijalishi upo busy ukirekodi, kwenye tour, au ukiwa nyumbani na wasiwasi jinsi gani utapata fedha za kufanya video mpya – fanya kitu (haijalishi kiwe kidogo vipi) kuwafikia mashabiki wako.
Kila siku – haijalishi upo busy ukirekodi, kwenye tour, au ukiwa nyumbani na wasiwasi jinsi gani utapata fedha za kufanya video mpya – fanya kitu (haijalishi kiwe kidogo vipi) kuwafikia mashabiki wako.
14. Kutoa video iliyo chini ya kiwango cha ukubwa wa wimbo
Video inafahamika kwa jinsi inavyoupa
uhai wimbo. Kama ukifanya video nzuri ya hit yako, basi ukubwa wa wimbo
utaongezeka mara dufu. Lakini kama ukifanya video ya kawaida ama iliyo
chini ya kiwango cha ukubwa wa wimbo, video hiyo itaichimbia kaburi refu
ngoma hiyo.
Makala imeandikwa na Bongo 5

No comments:
Post a Comment