17 February 2014

KINANA ASUKIWA MIKAKATI YA KUMHUJUMU KISIASA

IMG_2372Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kushoto akiwa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi jijini Mbeya hivi karibuni
NA MWANDISHI WETU, Dodoma
WAKATI Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha kazi ya kuwahoji baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotajwa kuanza mbio za kusaka urais 2015, kabla ya muda, zimeanza kuvuja fununu za najama za kusukwa hujuma dhidi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana na Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula.
Hujuma hizo ni kutoka kwa moja ya makundi ya mitandao ya wasaka urais, ambayo mgombea wao mtarajiwa ni kati ya waliohojiwa kwa muda mrefu kuanza kampeni mapema.
Waliohojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM ni;
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Uhusiano na Uratibu Steven Wassira na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wengine ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Januari Makamba na Mbunge wa Sengerema William Ngereja.
Hujuma dhidi ya Kinana zinakwenda mbali zaidi huku wasiwasi ukitanda huenda hadi hujuma hizo kuweza kufanikiwa, Kinana atakuwa amelipa gharama kubwa na hatima yake inaweza kuwa kitendawili kizito siku za baadaye.
Chanzo cha habari cha uhakika kutoka kambi inayotajwa kuhusika na hujuma hizo kinaeleza kwamba kinachomponza Kinana ni ujasiri usiotarajiwa
alioonyesha kiasi cha kumudu kumshawishi Rais Jakaya Kikwete, kuridhia awahoji ‘wagombea urais’, ikielezwa kwamba ujasiri wa Kikwete binafsi si wa kiwango hicho hususan kwa wanasiasa wanaotajwa kuwa rafiki zake.
“Kuna mambo kadhaa yanayomponza Kinana kwa sasa na kwa kweli amekwishatambuliwa rasmi adui wa kambi mojawapo ya urais. Tangu achukue nafasi ya Katibu Mkuu amekuwa akifanya ziara za kujenga chama mikoani, ziara hizi zimepokewa vizuri kiasi cha si tu kumjenga Kinana kisiasa lakini kukwamua haiba ya chama iliyofifia. Kwa hiyo, Kinana sasa anakuwa kiongozi mwenye ushawishi zaidi si tu CCM bali hata katika kada mbalimbali za kijamii, kuanzia wasomi hadi viongozi wa dini.
“Pili, hotuba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa Chama, Mjini Mbeya, kwa sehemu kubwa alimsifu Kinana. Huu ni uthibitisho mwingine kwamba nguvu za Kinana katika CCM ni kubwa sasa. Lakini kubwa zaidi linalomponza na mbali ni la tatu ni kukataa kuwa na bei, hanunuliki wala kuhongwa na hapa kundi fulani la urais kwa sababu linaamini katika nguvu ya fedha, Kinana ni kikwazo kikubwa mno kwao,” kilieleza chanzo hicho cha habari.
Ni kutokana na hayo, chanzo chetu cha habari kinadokeza mambo matatu yanayoweza kutekelezwa na kundi hilo dhidi ya Kinana na Mangula, ambao ushawishi wa nguvu ya fedha kwao ni sawa na kile chanzo cha habari kimeita “upuuzi”.

Mpango namba moja
Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, mpango namba moja ni kuunganisha nguvu kwa mawaziri walioitwa mizigo. Mawaziri hao wanapangwa kujitokeza hadharani ili kumkabili Kinana, wakimlaumu katika mwelekeo wa kumjengea chuki dhidi ya wanaCCM, kwamba amewadhalilisha bila kujali kuitwa kwao mizigo msingi wake ni hoja za wananchi waliokutana na akina Kinana katika mikutano ya hadhara.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname