UNAFIKI, kubaguana na upendo wa maigizo vimeendelea kuonekana
miongoni mwa mastaa wa Bongo baada ya hivi karibuni kususa hafla ya
kumtoa nje mtoto wa mwigizaji machachari, Rose Ndauka aitwaye Naveen.
Tukio
hilo lilishuhudiwa na kamera za Risasi Mchanganyiko, lilitokea wikiendi
iliyopita, nyumbani kwa msanii huyo, Tandale – Tanesco, Dar, ambapo
kichanga chake kilikuwa kimetimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwake.
Tofauti na matarajio ya wengi, hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa wachache ambao hata hivyo baadhi yao hawakuonesha ushirikiano wa kutosha – ni kama walikwenda kutembea tu!
Wengi kati ya wachache waliohudhuria walijifungia ndani, wakikwepa macho ya watu badala ya kusaidiana majukumu ya hapa na pale kama ilivyotegemewa.
Wasanii walionekana kuwa bize kumuunga mkono mwenzao ni pamoja na Yvonne Cherry ‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’, Chuchu Hans na Skaina Ally. Risasi Mchanganyiko lilimwuliza Rose kuhusu kususwa huko ambapo alijibu: “Siwezi kusema wamenisusia, unajua wakati mwingine huenda wametingwa na majukumu. Nilichokifanya ni kutimiza wajibu wangu wa kuwaalika wenzangu na nilitegemea wangenisapoti.
“Hata hivyo wapo baadhi walitoa udhuru mbalimbali. Nimefurahi kwa waliofika na nimefarijika sana kuja kusherehekea pamoja nami. Nawapenda wote maana ni ndugu zangu

Akaongeza: “Pia siwezi kuacha kumshukuru mama yangu mzazi pamoja na
mama mzaa chema (mkwewe) kwa kunipa sapoti katika kipindi chote
nilichokuwa mjamzito mpaka nilipojifungua salama... jamani mimba siyo
kitu kidogo.”
No comments:
Post a Comment