Unaambiwa
kwenye mji wa Berlin huko Ujerumani kwenye supermarket tano
yamepatikana mabox yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikua na dawa za
kulevya zilizofichwa ambazo ni kilo mia moja arobaini.
Ni
kosa ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa
wenyewe manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza
matunda kwa jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa
meli kutokea Colombia.
Wafanyakazi
wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo ndani yake ndio
kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa kadhaa baada ya
ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.
Polisi
wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia
sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti
kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.


No comments:
Post a Comment