Muigizaji wa kike Jacqueline Wolper aka Wolper Gambe ambaye
anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na
kucheza uhusika wa msichana ‘nunda’ ama mkatili, anajiandaa kuachia
filamu aliyoipa jina ‘Tom Boy’ ama ‘Jike Dume’.
Wolper Gambe amesimulia kwa ufupi kupitia Instagram jinsi alivyouvaa
uhusika katika filamu hiyo akiwa kama ‘Jike Dume’ aliyeamua
kujimilikisha msichana mwenzake lakini mwisho wa siku yeye mwenyewe
aliishia mikononi mwa mwanaume wa kweli na kupewa ujauzito kiulaini.
“Ni kazi mpya ni kali sana aipotoshi bali yaelimisha.nilijihi
mwanaume nikamilik dem lkn kumbe mwanamke ni mwanamke tuu nikaja kupewa
mimba nakuolewa na huyo kaka hapo.so kwa wale wenzangu fanaofanya
fanyeni lkn kumbuken kuna wanaume na ndo maana mungu kaumba kike na
kiume.hii movie inaelezea kila ktu ikitaka kutoka nitawajulisha stay
kunogewaaa mambo binafs follow @wolpergambe hii acc yakazi tu.” Ameandika Wolper Gambe.
No comments:
Post a Comment