24 January 2014

HILI NDO GARI LA KWANZA KUTENGENEZWA AFRIKA

Picha na Nairaland.com
Gari la kwanza kabisa kutengenezwa Afrika lilitengenezwa huko nchini Nigeria na kupewa jina Izuogu600. Kwa mujibu wa wikipedia, IZUOGU Z600 lilitengenezwa kwa vifaa ambavyo 90% ya vilitengenezwa hapa hapa Afrika, huko nchini Nigeria.
Hata hivyo gari hilo lililogunduliwa na Dokta Ezekiel Izuogu, wa huko Nigeria leo hii halipo sokoni baada ya kile anachodai mgunduzi huyo "fitina" na kutokupenda maendeleo kwa baadhi ya watu nchini kwake, kama alivyonukuliwa na imostateblog
Kilichotokea ni kuwa uzalishaji wa magari kama  hilo ambalo lilibuniwa mwaka 1997 na vifaa vyake kutengenezwa huko huko Nigeria, ulishindwa kuendelea kwakuwa majambazi wenye silaha walivamia kiwanda cha Dr. Izuogu tarehe 1 Machi 2006 na kuiba vifaa vyote  muhimu vya uzalishaji wa gari hilo pamoja na vitabu vya jinsi ya kutengeneza gari hilo.
Wakati wizi huo unafanyika, Dr. Izuogu tayari alikuwa amekwisha pata "mchongo" wa kuruhusiwa kuanzisha kiwanda nchini Afrika Kusini cha kutengeneza magari hayo ya Izuogu -Z600.
Kwa mujibu wa Dr. Izuogu mwenyewe ambaye alitumia miaka mingi kubuni gari hilo ni kuwa wizi uliofanyika kiwanda chake ulivunja matumaini yote ya ndoto yake kukamilika.
Hata hivyo wapo watu huko Nigeria wanaomlaumu dokta huyo kwakuacha yeye mwenyewe wazo lake life. Wengine wanalaumu chuki za kimaendeleo miongoni mwa waAfrika wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname