22 January 2014

H BABA AFUNGUKA YA OYONI KUWAHUSU DULLY, TID, Q CHIEF NA WASANII WENGINE. SOMA ALICHOKISEMA HAPA.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicnMyFF5F2oJuaoWfkWB7NOu9RkzavGg9nHTY8lUo2QG3bVQeLC6xeCKm-gl2Q-dWsN0XM0uDPCYP8pSyxK8wCv2Udx3PmMEAK121RoB4qoI57lXWoF2UUCLoaOare3se_d4wVcwJEtC8/s400/h-baba.jpgAsubuhi ya leo tuliandika post kuhusu umuhimu wa kushukuru, ambapo katika post hiyo tulielezea jinsi msanii The Rock alivyoamua kumshukuru mfanyakazi wake wa ndani aliyekaa nae kwa zaidi ya miaka 10 kwa kumnunulia gari moja kali sana.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWkuuxdghDHhgjhzdo-t3nywSSAxEdmY5aM2NJgW0CsdbeOozoRTjWdi7kxoX44IYGeScLk15QtEJ1I3aZIjcqWyBul3bofw5cbzpVc8nv1RKEGDfGczp9hhiAXeorcvlwjAXktnM9z-U/s640/DULLY-SYKES.jpg
Sasa jioni ya leo msanii H Baba kaamua kutoa shukrani kwa wasanii mbalimbali waliochangia kuufikisha mziki wa Bongo Flava hapa ulipo leo. Msanii H Baba kaamua kumwaga shukrani nyingi sana kwa msanii Dully Sykes kwa kumwelezea kama mtu aliyechangia vitu vingi sana katika mziki huu wa Bongo Flava. Hiki ndo alichokiandika msanii H Baba katika moja ya post zake kwenye mtandao mmoja wa kijamii "King wa bongo flavour muasisi wakuimba bongo . Namkubali sana mwanamuziki huyu apa #anaroho yakusaidia sio mchoyo #mkalimu Kwa watu wote #nimshauri mzuri sana kama unaonaujielewi mtafute dullysykes nimsaada mkubwa Kwa wasanii wabongo flavour . Upande Wangu dully kanisaidia mambo mengi yanayousu sanaa sio mchoyo wamwenzie akapate #salute broo . Bongo flevour kunaherufi zako ndani zinakuhusu nakuheshimu Bila nyinyi kaka zetu kuusogeza mziki wetu Leo sijui ningekuwa wp? Nawaheshimu sana wasanii waimbaji kaka zangu kiumli mpaka kimuziki mimdogo wenu tuu. Hawa apa wapo vitani bado kaka zangu wamuziki top in dar #T I D . dullysykes Mr misifa bananazorro Mr.Nice mfalme wa takeu Q chillah savimbi #big up kwenu kwakutuleta mjini wasanii wamikoani.."
 
Timu nzima ya Bongoclan inapenda kumpongeza na kuwapongeza wasanii wote waliotajwa na H Baba kwani ni ukweli usiofichika kua wameleta maendeleo na kufanya kazi kubwa sana katika kuutambulisha mziki wa Bongo Flava ndani ya Tanzania na hata Kimataifa. Mlifanya mziki tangu kipindi kile malipo yakiwa kiduchu lakini hamkukata tamaa mpaka leo tunaona maendeleo makubwa katika mziki huu ambapo tumeona mafanikio kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongo Flava. Mungu awabariki sana
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname