11 November 2013

WATU bwana! SOMA aliyoambiwa Irene UWOYA baada ya kusema ANATAMANI kuigiza na Nicolas Cage...SOMA VIHOJA HIVI


mwigizaji wa bongo movies Irene Uwoya amefunguka na kudai kuwa anatamani sana kufanya kazi na mwigizaji wa kimataifa toka marekani Nicolas Cage siku moja.

Mrembo huyu ameongea na bongomovies na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kutamani kufanya kazi na mwigizaji huyo ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuigiza na pia uzoefu wake katika tasnia ya filamu duniani.


Nicolous Cage amejipatia umaarufu sana kwenye tasnia ya filamu Marekani na duniani kote kuotkana na filamu zake mbalimbali kama “National Treasure”, “Ghost Rider” ,“The Frozen Ground” na nyingine nyingi.

Kama kawaida mashabiki nao hakakuwa nyuma kutoa maoni yao juu ya kauli ya mwanadada huyu na baadhi yao walimpa moyo kuwa inawezekana kwa kumwambia….

 “Ipo siku zitatimia ndoto zako kaza buti…”
“ Muomba Mungu hachoki mpenzi wangu…”
 “One day Yes”
   “Mungu akupe uzima ndoto zitatimia”
“Kwamungu kila kitu kinawezekana usijali ipo siku…”


Na wengine kama kawaida walimwambia bado sana, ajipange kwanza….


 “Nicholas Cage.sasa yeye movies zake za mbilinge sana we mlaini sana hutoweza “
“ Nicolas cage u got a wrong way to mamy kila kitu kinawezekana…”
“…Labda uwe.umetekwa alafu anakuja kukuokoa…”
“Nackia ngeli hujui....xa mtafanyaj kaz???, alihoji shabiki mmoja


Na wachache waliokuwa nje ya mada kabisaaaa kwa kuandika…

“…Nataman angekua mume wangu…” 



Na Wewe unaonaje? Inawezekana Irene akafanya kazi na Mwigizaji huyu? FUNGUKA HAPO CHINI MDAU

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname