Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao.
Kata ya mafiga wa upande wake ilionekana kutekwa kabisa na CHADEMA, huku katika mkutano wa Ndani Afande Sele alichaguliwa kushika nafasi ya Uenyekiti wa kata hiyo, katika kipindi hiki cha kushusha chama kwa wananchi (Program ya Chadema ni msingi), ambayo imekuwa mwiba mkali kwa CCM.
No comments:
Post a Comment