Kwa kawaida kila binadamu anayop siri
yake moyoni ambayo hapendi hata siku moja ifahamike. Lakini kwa upande
wa wanaume haijalishi amekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda gani au
amejuana na mwanamke kwa muda gani hiyo haiwezi kuwa ni kigezo cha
kumuamini mpenzi wake kiasi cha kumweleza siri zake za moyoni. Kuna
uwezekano zipo atakazoficha kwa muda lakini hapo baadaye akaamua
kumweleza mwenzi wake, lakini kuna zile nyingine ambazo nitataja baadhi
ambazo kamwe mwanamke asitarajie kuona mpenzi wake akifungua kinywa
chake na kumweleza. Na hata ikitokea mwanamke akazijua kupitia kwa
wapambe, ni dhahiri mwanaume huyo atakanusha kwa nguvu zake zote na hata
aikibidi kutumia ubabe ili kuzima hoja hiyo..
Kwamba ana matatizo ya kifedha:
Inawezekana wakati anakutana na mpenzi wake mambo yalikuwa safi na
alikuwa na fedha za kutosha kula bata na kuishi maisha ya kifahari,
lakini kama ikitokea mambo yakageuka ghafla bila ya kutarajia kwa mfano
alikuwa na njia zake za panya za kupata fedha nje ya mshahara halafu
njia hizo zikafungwa na mshahara ukawa hautoshi kabisa kukidhi hata robo
ya mahitaji yake na mpenziwe, hapo mwanaume anaweza kutumia mbinu
mbalimbali ili kuweka mambo sawa, ikiwezekana hata kukopa ili kusitiri
aibu lakini si kumwambia mpenzi wake kwamba mambo yamegeuka, labda kama
ni mkewe, lakini si mpenzi ambaye bado mambo hayajaiva
Kwamba aliwahi kubaka au kumla mtungo
mwanamke na marafiki zake wakati fulani: Inawezekana historia yake ya
ujana ilikuwa na vibweka vingi ikiwemo kubaka wanawake au kufanya
mapenzi na mwanamke mmoja akishirikiana na marafiki zake vijana wa mjini
huita mtungo au kula mande. Mwanamke asitarajie mwanaume atafungua
mdomo wake na kuelezea huo upuuzi wake.
Kukiri kwamba alikudanganganya ili
akupate: Kuna wakati mwanaume hulazimika kudanganya au kuingia na gia
kubwa kama vijana wa mjini wanavyosema ili kumpata mwanamke wa aina
fulani. Kuna baadhi ya wanawake wamejiwekea viwango vya aina ya wanaume
watakaopenda watoke nao, shida ni pale kina Bujibuji watakapokuwa
wamefika bei lakini tatizo viwango viko chini, hapo ndipo mbinu na
mikakati vitatumika ikiwezekana kujivika uhusika asiokuwa nao ili mradi
ampate huyo mwanamke, na akimtia mikononi halafu mwanamke akashtukia
kwamba ameingizwa Kingi na kujaribu kuhoji, asitarajie mwanaume huyo
atakiri udhaifu. Lazima atajitahidi kutafuta namna ya kukwepa kuonekana
muongo ili mradi kulinda hadhi yake ya uongo
Kukiri kwamba aliwahi kufungwa jela na
kulawitiwa: Inawezekana mwanaume aliwahi kufungwa jela, lakini kama
inavyojulikana misukosuko ya jela ni mingi ikiwemo kuingiliwa kinyume na
maumbile, au inawezekana mwanaume katika mazingira fulani aliwahi
kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kulazimishwa katika mazingira magumu
na ya aibu. Kamwe mwanamke asitarajie kwamba mwanaume huyu atakuja
kufungua mdomo wake na kumweleza mwanamke kuhusu jambo hilo. hata akija
kulisikia mwanaume huyo atalipinga kwa nguvu zake zote.
Mwanaume kukiri kwamba alikuwa
ANASAFISHA KIWI CHA MACHO: Hata kama akikamatwa live na mpenzi wake
akisafisha kiwi cha macho, si rahisi mwanaume akubali huo udhaifu, ni
lazima atapinga kwa nguvu zake zote.

No comments:
Post a Comment