11 November 2013

RAY C ..ASHEREKEA MWAKA MMOJA TANGU AACHE MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA

Ray C: Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana

Rehema Chalamila aka Ray C haisahau kabisa tarehe 8/11/2013 kama siku ambayo aliachana rasmi na matumizi ya dawa za kulevya na kupewa tiba kwa msaada wa rais Jakaya Kikwete.
Ray C aliitumia siku hiyo kuungana na watu walioacha kutumia dawa za kulevya, na kwa pamoja walijipongeza kwa hatua hiyo.

Kupitia Instagram, juzi (November 8) Ray C alipost picha akiwa na watu hao na kuandika ujumbe kuonesha upendo wake kwao, na kwa kuona watu wanaweza kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo anaamini Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.
“@ Nawapenda sana hawa wenzangu wote tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa Tumepona na tunamshukuru Mungu....Tanzania bila Madawa ya Kulevya inawezekana.”  
Baada ya kumaliza kupeana pongezi na elimu zaidi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C aliielezea siku hiyo kupitia Instagram.
“Looooong day but am very happy....8/11/2013 Will always remember ths special Day......God!I heart You....” aliandika Ray C

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname