18 November 2013

"NIMEAMUA KUACHA KUJICHUBUA"...MAINDA

 
  STAA mwenye umbo la kipekee katika soko la filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa ameamua kuukacha mkorogo aliokuwa akiutumia kwa muda mrefu.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema ameamua kuacha kutumia mkorogo kutokana na matakwa ya dini yake, amegundua anamkosea Mungu wake kwa kujichubua . Nimeamua tu kuacha kujichubua, mkorogo siyo kitu kizuri hata Mungu hapendi vitu hivi ndiyo maana nikaamua kuuacha japo nimetumia kwa muda mrefu,” alisema Mainda ambaye kabla ya kuokoka alikuwa Muislamu.
CREDIT: GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname