07 November 2013

MBEYA CITY YAFANYA KUFURU DAR...YAJA NA MABASI 10 TOKA MBEYA ,JIJI ZIMA LA DAR MAONGEZI NI MBEYA CITY DHIDI YA AZAM


Timu ya Mbeya City imepeleka mashabiki zaidi ya 300 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuizima Azam FC kwenye mechi ya leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Chamanzi.  

MBEYA City imefanya kitu ambacho hakuna timu ya mkoani iliwahi kufanya katika miaka kumi iliyopita kwenye Ligi Kuu Bara.
Timu hiyo imepeleka mashabiki zaidi ya 300 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuizima Azam FC kwenye mechi ya leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Chamanzi.
Uongozi wa Mbeya City umekiri kwamba unatambua na unasapoti ya mashabiki hao kwenye mechi hiyo ngumu ambayo itaamua timu ipi itaongoza ligi mpaka mwakani kwani Azam na Mbeya City kila moja ina pointi 26.
Timu hizo zote zipo sawa kwa kila kitu kasoro idadi ya mabao ya kufunga tu, kwani zote zimecheza michezo 12, zimeshinda  michezo saba, zimetoa sare michezo mitano na hazijapoteza hata mchezo mmoja na zimefungwa mabao saba kila mmoja na utofauti wao ni  Azam imefunga mabao 20 wakati Mbeya City imepachika wavuni mabao 16.
Kiongozi wa tawi kubwa la klabu hiyo lililopo Mwanjelwa jijini Mbeya, Wille Mastala aliliambia Mwanaspoti kuwa orodha aliyonayo inaonyesha mashabiki ni zaidi ya 300 wamejiorodhesha kwa safari ya Dar es Salaam.
“Tumejipanga na tunauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa kwani tumeona jijini Mbeya timu inasapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, kwa nini ugenini tusiisapoti ndio tukajipanga na kuamua kuja Dar es Salaam ili kuhakikisha Azam anakufa  Alhamisi kwa mabao 2- 0,” alisema.
“Tumekodi  mabasi 10 kwa  ajili ya mashabiki ili kuisapoti timu, tumefunga safari ya saa 12 kutoka Mbeya kuja Dar  kuishangilia timu,” alisema Mastala huku kocha wa timu hiyo, Juma Mwambusi akiahidi kupambana kiume uwanjani.
Mbeya City imekuwa ikisafiri na idadi kubwa ya mashabiki kila inapokwenda nje ya mkoa na kishindo cha shangwe kimekuwa kikisikika zaidi inapokuwa katika uwanja wake wa Sokoine.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname