Mchungaji Daniel Kisonga akimwonyesha mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe
Mbwa huyo akinyonyesha watoto wa Nguruwe huku mtoto wake (kulia) akishindwa kunyonya
Huyu ndie Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa
Katika hali isiyo
ya kawaida kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala katika Manispaa ya
Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya kushuhudia tukio la
aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa nguruwe na kuwalea kwa
kuwanyonyesha maziwa yake.
Tukio hilo
limetrokea machi 15 mwaka huu majira ya asubuhi baada ya nguruwe wa mmoja kati ya
watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel Kisonga kushuhudia mbwa huyo
ambae alikuwa amezaa watoto watatu na kufariki wawili na kubakia na
mtoto mmoja na hivyo kulazimika kuingia katika banda la nguruwe na
kubeba watoto wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa huduma
zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa upendo watoto hao wa Nguruwe
bila kuwadhuru.
Akizunguza na mwandishi wa habari hizi leo mchangaji
Kisonga amesema kuwa ni vigumu kuamini kuna mbwa akinyonyesha
watoto wa nguruwe wakati kwa kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari
kwa nguruwe hao hasa pale wanapozaliwa .
Amesema kuwa mbwawa
wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada
ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti kwa mbwa baada ya
kuamua kulea watoto wa nguruwe .
Hata hivyo amesema
yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni dalili za siku ya
mwisho kama ambavyo zimepatwa kutabiliwa katika maandiko matakatifu
kuwa siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo binadamu
ni vigumu kuamini mambo hayo.
credit : francis godwin
No comments:
Post a Comment