28 November 2013

ADAM JUMA AVUNJA UKIMYA AFUNGUKA NA KUMWAMBIA NISHER "ASITAFUTE USTAA KWA CHATU ALIYELALA".......SOMA HAPA ZAIDI

Muongozaji mkongwe wa video, Adam Juma  ameamua kujibu ujumbe wa kejeli alioandikiwa na muongozaji wa video aliyekuja juu nchini, Nisher.

Nisher alipost picha yenye maneno yanayoonekana kuwa dongo kwa Adam Juma ambaye anaaminika kuwa na mchango mkubwa katika kubadilisha muonekano wa video za muziki za Tanzania.
Kwenye picha hiyo, Nisher aliandika: I’m not next level, I’m a new game’.
‘Next Level’ ni jina la kampuni ya Adam Juma.
Ujumbe huo ulimkera Adam aliyesema kuwa Nisher anamtafuta na kumwambia kuwa asianzishe vita ambayo hawezi kuimaliza.
“Afanye kazi yake asitafute ustaa kwa chatu aliyelala. Ajitahidi wasanii wasiende Ogopa basi. Changamoto my ass. Ukimya si upuuzi but ni busara, sijapenda hii msg, but anyway I got something for you,” aliandika Adam kwenye Instagram.
“On that note atafute mchiriku na mduara mmoja tuone creativity. In the end if you good I will respect you.” Aliongeza Adam Juma.
VIA HOT NEWS DAILY

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname