29 October 2013

ANGALIA MJUMBE ALIVYOZIMIA KISA KUHESABU KURA ZAKE




Kaimu meneja wa zamani wa Yanga, Ayoub Nyenzi alizimia mara baada ya kugundua kuwa alikuwa ameshinda ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF katika mikoa ya Mbeya na Iringa.




Nyenzi alizimia baada ya kuamua kuhesabu kura zake mwenyewe na kugundua alikuwa ameshinda.







Mara tu baada ya kugundua ameshinda, Nyenzi aliangusha kilio cha nguvu kama mtu aliyepoteza nafasi hiyo.



Baadhi ya waliokuwa katika chumba hicho cha mikutano cha Ukumbi wa Water Front walionekana kutoelewa wakidhani amepoteza.







Lakini walielelezwa alikuwa akilia kutokana na kugundua kwamba ameshinda na hakuchukua muda kabla ya kuanguka na kuzimia.



Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya ambaye alikuwa kati ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo, alitoa huduma ya kwanza kwa Nyenzi aliyekuwa hajitambui kabisa.


Hata baada ya kupata fahamu, bado Nyenzi alionekana haamini kilichotokea na kuendelea kumwaga chozi huku akiangusha kilio cha furaha

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname