KASEJA (MWENYE KOFIA) AKIFUATILIA MECHI UWANJA WA TAIFA. MBELE YAKE MWENYE NYWELE ZENYE RANGI NI UHURU SELEMANI |
Katika
kipindi cha miaka kumi sasa, kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja
aliingia kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa kama shabiki.
Kaseja
aliyekuwa nahodha wa Simba, aliachwa katika kikosi hicho kwa madai ya
kushuka kiwango ingawa kila kitu kinaonyesha zilikuwa ni chuki binafsi.
Katika mechi ya jana iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3, Kaseja alionyesha vitu kadhaa muhimu ambavyo vinaweza kuelezewa.
Pamoja na kuachwa kwa chuki binafasi, lakini alionyesha hana chuki na Simba na kwenda kukaa katika jukwaa la mashabiki wa Simba.
Achana
na hivyo, Kaseja alizidi kuonyesha yeye ni Simba damu kwa kuwa kama
ingekuwa tofauti angeweza kwenda kukaa jukwaa la Yanga aliyowahi
kuichezea kwa mwaka mmoja.
Tatu,
akiwa na Uhuru Selemani ambaye pia aliwahi kuichezea Simba, Kaseja
alionekana si mpenda makuu kwani alikaa sehemu ya kawaida na akaonyesha
utulivu si kama walivyo wachezaji wengine nyota.
Wakati
Simba ikishindiliwa mabao katika kipindi cha kwanza alionekana kama
alikuwa anawaza kitu fulani, angalau katika kipindi cha pili, tabasamu
lake lilianza kuonekana.
No comments:
Post a Comment