MIEZI kadhaa imekatika tangu msanii wa filamu za Kibongo, Jimmy
Mafufu afunge ndoa ya Kiislamu lakini cha kushangaza ameibuka na kusema
hakubadilisha dini isipokuwa aliigiza ili apewe mke.
Jimmy
aliweka bayana juu ya ishu hiyo hivi karibuni alipokuwa kwenye msiba wa
muasisi mkuu wa makanisa ya EAGT, Moses Kulola ambapo alisisitiza kuwa
kamwe hawezi kubadilisha dini kwani amezaliwa na kukulia katika familia
ya kilokole na
aliyekuwa akimlea ni marehemu kiongozi huyo.
“Babu
yangu mzaa mama ambaye ndiye ameachwa mrithi wa Kulola na alikuwa pia
msaidizi wake, Askofu Mwaisabila walikuwa marafiki sana na muda mwingi
nilikuwa nikikaa nyumbani kwa Kulola hivyo nimedumu katika misingi ya
Kilokole,” alisema Jimmy huku akisisitiza kuwa hata filamu nyingi
anazocheza zina maudhui ya dini.
No comments:
Post a Comment