Rubani wa British Airways ametumia nafasi yake kudhalilisha mamia ya watoto wasio salama kwenye shule za Afrika na vituo vya kulelea watoto, Daily Mail limefichua.
Ofisa
wa Kwanza Simon Wood, mwenye umri wa miaka 54, alidai alikuwa akifanya
kazi za kujitolea kwa niaba ya shirika hilo la ndege huku
akiwadhalilisha wengi wa wasichana wadogo wakati wa vituo vyake barani
Afrika.
Akivalia
sare bandia za rubani, alitumia sifa nzuri za shirika hilo - na hata
wanasesere waliowekwa nembo za shirika hilo na vitabu vilivyopakwa rangi
za shirika hilo - kushawishi watoto kwenye safari za mchana na kwenye
hoteli za nyota tano zinazotumiwa na shirika hilo la ndege, ambako
aliwadhalilisha.
British
Airways sasa inakabiliana na mashitaka yanayoibomoa kwa kiasi kikubwa
yaliyowasilishwa na waathirika wake, ambao wanasema kampuni hiyo
imeshindwa kuwalinda kutokana na udhalilishaji wake wa kutisha.
Baada
ya kuwadhalilisha watoto kwa miaka 15, rubani huyo anayelipwa Pauni za
Uingereza 100,000 kwa mwaka hatimaye aliacha pale aliposhitakiwa kwa
mashitaka tofauti ya kushiriki ngono na watoto nchini Uingereza.
Siku
kadhaa baada ya kufikishwa mahakamani mjini London mwezi uliopita
akishitakiwa kwa makosa hayo, Wood alijitupa chini ya treni.
Mwendesha
mashitaka Peter Zinner alisema: "Upande wa mashitaka unasema kwamba
Wood alikuwa amepotosha kwa kina na kuwahonga watu ambao alitumia uwezo
wake wa kuruka kwenda sehemu nyingine za dunia kufanya makosa ya
kujamiiana dhidi ya watoto."
Maofisa
nchini Kenya wamewatambua takribani watoto 15, wote wanaaminika kuwa
wasichana wenye umri wa kati ya miaka mitano na 11, ambao Wood
aliwadhalilisha - na kusema wanahofia kuna mamia zaidi.
Wakati
British Airways imeanzisha uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na tuhuma
hizo za 'kushitusha', maswali yameulizwa kuhusiana kwanini rubani huyo -
ambaye alikamatwa baada ya shambulio lisilo sahihi kwa msichana wa
miaka minane mwaka 2000 - aliruhusiwa tena kufanya kazi karibu na
watoto."
Vyanzo
vya upande wa mashitaka vilisema vinahofia rubani huyo anaweza
kuthibitisha kuwa miongoni mwa wahalifu wa makosa ya kujamiiana.
Katika
utumishi wake wa miaka 16 akiwa British Airways, Wood alichagua safari
zisizo maarufu ndani na nje ya Afrika Mashariki, akitumia kukaa kwake
huko kuwinda watoto wasio salama katika mitaa ya ovyo.
Mawasiliano
yake ya kwanza na watoto yanayofahamika katika Afrika yalifanyika mwaka
2001 pale alipoanza kutembelea kituo cha kulelea watoto kilichoko eneo
la Karen huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Wakati
wa Pasaka 2002, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi 20 kutoka ndege mbili
za British Airways ambao walijitolea kutumia mapumziko hayo na vijana
hao wa Kenya, kukijaza kituo hicho kwa zawadi lukuki, dawa na michango
iliyochangwa kutoka Uingereza.
Alilieleza
shirika la habari la Uingereza la Press Association, ambalo liliripoti
safari hiyo: "Tunacheza, kuimba, kufanya kazi mbalimbali na kwa ujumla
kuwaburudisha. Tumekuwa karibu mno na watoto hao."
Kwa uhalisia Wood alikuwa akitumia hadhi kubwa ya sare zake za urubani kuweza kuwafikia watoto kwa malengo ya kuwadhalilisha.
Matukio
mengi ya hivi karibuni ya udhalilishaji yametokea wakati wa kituo chake
Uganda, kituo cha mwisho cha safari yake ya kawaida, kutoka ambako
alivuka mpaka huo kwenda nchini Kenya kuwalenga watoto walioko katika
mitaa ya ovyo na yatima.
Maofisa
nchini Kenya wanasema, alidai alikuwa mshirika wa 'mpango wa British
Airways wa uhusiano wa jamii' wakati akiingia kwenye vituo vya kulelea
watoto na mashule.
Kama
mameneja wakilalamika kuhusu tabia yake, Wood alifungua malalamiko
rasmi kwa polisi kwamba wafanyakazi waliohusika walikuwa wakiiba kutoka
kwenye nyumba za watoto hao, na takribani mameneja wawili walikamatwa
kuhusiana na madai hayo.
Wood
kwanza alifikishwa polisi pale alipotuhumiwa kwa tukio la shambulio
dhidi ya binti wa miaka minane. Alikutana na binti huyo wakati
akijitolea kwa maradhi ya Kisukari nchini Uingereza, akisindikiza watoto
wadogo katika safari ya kwenda North Yorkshire mwaka 2000.
Wood
alikamatwa kuhusiana na ubakaji, lakini - kama ilivyokuwa kwa skendo la
Jimmy Savile - Waendesha Mashitaka wa Mahakama Kuu waliamua hakukuwa na
ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Aliruhusiwa kuendelea na kazi yake
British Airways na, akaendelea na kazi yake ya kujitolea kwa watoto.
Mama
wa mmoja wa waathirika hao wadogo alieleza binti yake alidhalilishwa
kwenye hoteli moja ya nyota tano inayotumiwa na wafanyakazi wa British
Airways mjini Nairobi.
Alisema
kwamba baada ya kumkopesha pesa Wood alimdanganya kumwezesha kumpeleka
binti huyo wa miaka mitano kwenye hoteli ya Nairobi Intercontinental.
"Nilimwamini kupita kiasi sababu alionekana mwema sana na mkarimu. Nilimwamini kwa kila kitu, hata kwa binti yangu," alisema.
Msichana
huyo, sasa miaka 14, anahangaika shuleni na amekuwa akitokwa machozi na
kutengwa. Alitishia kujiua kuepuka aibu na maumivu aliyosababishiwa na
Wood.
Pale
mashaka yalipoibuka kuhusu Wood nchini Kenya, moja ya shule
ziliwasiliana na kampuni ya wanasheria Uingereza, ambayo mfanyakazi wake
alisafiri kwenda Kenya akiwa na mtazamo wa kuanza hatua za kisheria
dhidi ya Wood na British Airways.
Lakini walipobaini ukubwa wa makosa ya kujamiiana ya Wood dhidi ya watoto hao walipeleka suala hilo kwa polisi wa Uingereza.
Kufuatia
kutonywa, maofisa wa Uingereza walimkamata tena Julai 18 kwenye
maegesho ya magari ya wafanyakazi wa British Airways katika uwanja wa
Heathrow kuhusiana na shambulio la mwaka 2000.
Walipopekua
kompyuta zake za mapajani, walikuta picha chafu za vijana wa Kiafrika.
Wakati wa msako wa polisi wa gari la Wood sare kadhaa za shule zilikutwa
humo, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Westminster ilielezwa.
Mwendesha
Mashitaka Zinner alisema: "Kompyuta yake inashikiliwa na ushahidi
ulipatikana kuonesha kwamba alitembelea mitandao kadhaa ya udhalilishaji
dhidi ya watoto."
Wood
alifikishwa mahakamani Agosti 16 akishitakiwa kwa kumiliki picha chafu
na shambulio lisilo sahihi kwa mwanafunzi wa kike mwenye miaka minane.
Aliachiwa
kwa dhamana kwa sharti la kusalimisha pasipoti yake lakini siku mbili
baadaye alijitupa chini ya treni lililo kwenye kasi karibu na nyumbani
kwake huko Potters Bar, Hertfordshire.
Waendesha
mashitaka walitangaza Jumatano iliyopita kwamba kutokana na kifo chake,
walikuwa wanafanya taratibu za kusimamisha kesi hiyo.
Jennifer
Swiddon, anayemwakilisha Wood, alisema kwamba mteja wake alikusudia
kukana mashitaka yote dhidi yake kabla ya kifo chake.
Kabla ya kifo chake, Wood alikuwa amehamisha Pauni za Uingereza 64,000 kwenda kwa wawakilishi wake wa kisheria barani Afrika.
Familia
ya kaka zake Wood, Nicholas, miaka 52, na Anthony, miaka 51, zilisema
ulikuwa 'wakati mgumu kwa familia nzima' na kukataa kuzungumzia suala
hilo
No comments:
Post a Comment