
Msichana
mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu
baada ya kuzomewa na kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la
soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu
wasamariawema kuingilia kati na kutumia nguvu kubwa ili kumwokoa na
kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.
Mwandishi
wetu Halfani Lihundi kutoka arusha alikuwapo katika sakata hilo na
ametuma taarifa hii iliyosema, watu walio shuhudia tukio hilo wamesema
wamechukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani
na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili
kukomesha tabia hiyo.
Kwa
upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za
heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa
gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo
inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za
kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
No comments:
Post a Comment