Ana sura na umbo zuri sana, na mvuto mkubwa sana kutokana na rangi yake nzuri ya ngozi…
Early life
Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988
katika hospitali ya ST. Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa
mwisho kuzaliwa katika familia yao yenye watoto wanne wa kike.
Alipata elimu yake ya primary na
sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es
Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za
kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.
Career
Wema alianza kuigiza rasmi mwaka 2007
alipoonekana kwenye filamu ya POINT OF NO RETURN ambapo halicheza kama
mke wa jamaa tajiri mchawi ambaye daima huua wapenzi wake wa kike kama
sadaka. Wema alifikiri angeweza kufa pia lakini aliamua kumwomba Mungu
na mwishowe alifanikiwa kuiokoa familia yake na yeye.
Pamoja na filamu hizi Wema ameigiza
kwenye filamu nyingine nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani,
Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa zilizompatia
umaarufu na mafanikio makubwa.
Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji
wema pia anakipaji kikubwa cha kuimba na pia alishawahi kushiriki
mashindano ya urembo na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo
mwaka 2006 na kujipatia zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4

No comments:
Post a Comment