Prince Dully Sykes amesema anamfananisha
hitmaker wa ‘Number 1’ Diamond Platnumz na marehemu Steven Kanumba kwa
jinsi alivyo na moyo wa kuthubutu katika mambo yake.
Dully Sykes alikuwa akiongea na Bongo5
kwenye uzinduzi wa video ya video mpya ya Diamond uliofanyika wiki
iliyopita kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Diamond ni namba moja kwasababu yupo
tayari kujitoka kwa kila kitu,” alisema Dully. “Naweza kumfananisha
Diamond na mtu kama Kanumba. Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua
nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini
ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye
tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.”
Pia Dully amesema mwishoni mwa mwaka huu
anatarajia kuiongezea vifaa vipya studio yake ‘4.12’ ili kujiimarisha
zaidi kwenye utayarishaji wa muziki ambao anasema kwa sasa anaufurahia
zaidi kuliko hata kuimba

No comments:
Post a Comment