Dillish Mathews & Abdi Guyo
Wiki
iliyopita wakati mshindi wa $ 300,000 za Big Brother The Chase Dillish
Mathews kutoka Namibia akifanyiwa mahojiano na mwandishi wa Namibia,
alisema anahamu ya kukutana na baba yake mzazi ambaye hawajawahi
kuonana.
Baada
ya siku chache kupita hatimaye jana (September 2) mwanaume aitwaye Abdi
Galgayo Guyo alijitokeza katika ofisi za Standard media Kenya na kudai
kuwa yeye ndiye baba mzazi wa Dillish ambaye binti yake anahamu ya
kumuona.
Guyo
alirekodiwa na kituo hicho na kutoa maelezo ya jinsi alivyokutana na
mama yake Dillish aitwaye Selma Pashukeni mpaka walivyompata Dillish na
baadaye kupotezana.
Bwana
Guyo ambaye ni askari mstaafu wa Kenya aliiambia Standard Media kuwa
alikuwa ni miongoni mwa maaskari wa Kenya wa kikosi cha kulinda amani
cha Umoja wa mataifa ‘United Nations Transition Assistance Group ‘,
kilichopelekwa nchini Namibia kuanzia (April 1989) mpaka (March 1990)
kusimamia mchakato wa amani pamoja na uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo na
huko ndiko alikutana na Selma.
Abdi
Guyo, alisema baada ya kukutana na mama yake Dillish Selma walipendana
na kumpeleka katika kambi ya jeshi walikofahamiana vizuri zaidi
kimapenzi mpaka Selma kubeba ujauzito wa Dillish, Guyo aliongeza kuwa
baada ya kurejea Kenya alikuwa akituma barua kwa Selma kabla ya kupoteza
mawasiliano.
Wiki
iliyopita Jumatano, Rinelda Mouton, mwandishi wa habari wa Namibia
alifanya mahojiano maalum ambayo Dillish na familia yake walitaka
kukutana na baba yake halisi.
Katika mahojiano hayo Dillish alisema mama yake aliwahi kumwambia kuhusiana na baba yake Mkenya.
Dillish mwenye miaka 22 alizaliwa mwaka 1991.

No comments:
Post a Comment