18 September 2013

AIBU KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA IFM WASHUTUMIWA KUVAMIA HARUSI ZA WATU..BILA HATA YA KUALIKWA.



Kuna harusi moja nilienda ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa Karimjee.Siku hiyo nilikakutana na mambo ya ajabu sana katika harusi hiyo eti wamekodisha kampuni ya ulinzi kusimamia kadi mlango, nikajiuliza hivi kweli harusi zetu zimefikia hatua hii?
Nilikaa ndani lakini kichwa kilikuwa kinanigonga sana kwa nini hali hiyo wakati mimi nimezoea mlangoni katika harusi nyingi nawakuta watu wawili tena wanakati wamevalia vizuri wanawakaribisha wageni kwa sura zilizojaa tabasamu.


Sikukubali kuzidi kuumizwa kichwa nikaamua kutoka mara moja nje kisha nikamuita askari mmoja nikamdodosa akaniambia hapa sisi tumekodishwa kuwadhibiti baadhi ya wanafunzi wa IFM ambao huwa wanakuja wamevalia vizuri kuvamia harusi ambazo zinafanyika hapo.

"Kaka wanafunzi hao ni hatari sana, ukimuona kavaa nguo zake utasema mtu wa maana sasa jaribu kumuuliza kadi iko wapi? utasikia anakuja nayo mke wangu oooh mara nimesahau watu kama hao sisi huwa tunawatimua, wako wengi sana"alisema mlinzi huyo.

Jamani wanafunzi wa IFM elimu mnayochukua na suala hili ni aibu. Najua sio wote ila kuna baadhi ndio wanawachafulia jina la chuo chenu wafichueni basi 
 source-http://www.natafutashule.com

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname