20 August 2013

TAARIFA ZA BILIONEA WA HOME SHOPPING CENTRE ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

Hakika aliyemmwagia tindikali bilionea Said Mohamed Saad, alifanya kitendo kibaya kupitiliza, kwani athari ambazo amemsababishia ni kubwa kiasi ambacho hata upatikanaji wa tiba mahsusi umekuwa wa kutangatanga.
taarifa za ndani na zenye uhakika kuwa Said ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, amekimbizwa Ujerumani kwa matibabu zaidi baada ya kushindikana Afrika Kusini alikopelekwa awali.
Said alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani Mall.
Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa tindikali, alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar es Salaam lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60, alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa Afrika Kusini.BOFYA HAPA KUISOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname