17 August 2013

MTANZANIA ALIYEKAMATWA LOS ANGELES AKIRI KUINGIZA HEROINE MAREKANI

Mtu aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).

Shirika la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi. 
Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.KUISOMA ZIDI BOFYA HAPA



No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname