24 August 2013

MADAWA YA KULEVYA CHINA KUMEKUCHA

CHINA kumekucha! Sakata la kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kulitafuna taifa, safari hii limechukua sura mpya baada ya askari nchini China kufanya oparesheni maalum ya kuwanasa wahalifu wa biashara hiyo haramu nchini humo.Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka China, baada ya vyombo vya habari kuripoti mfululizo juu ya mfumuko wa biashara hiyo, askari waliandaa mpango maalum wa kuwanasa watu wanaojishughulisha nayo.“Baada ya vyombo vya habari kuripoti sana juu ya kukithiri kwa biashara ya madawa kulevya, polisi wamecharuka na kufanya msako wa nguvu katika maeneo ambayo Watanzania na watu mbalimbali wa kutoka Afrika wanafikia hapa  China,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname