
Elly G mwigizaji wa filamu
MWIGIZAJI wa filamu anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu
Swahiliwood Elia Daniel ‘Elly G’ hivi karibuni alinisurika kupoteza uhai
wake baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya Gongo, msanii huyo
alikutwa na sakata hilo akiwa anarekodi filamu yao ya Kupa maeneo ya
Kibaha vijijini Elly G alikuwa yupo katika scene iliyomfanya atumie
pombe hiyo.
.

Elly G akiwa katika pozi.

Elly G katika pozi lake matata.
“Nilimuona Israel mtoa roho , siku hiyo nilikuwa nimekunywa dawa aina
ya Flagly na dawa nyingine kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na tumbo,
hivyo wakati narekodi kuna scene nilitakiwa ninywe pombe ya kienyeji
Gongo sasa unajua katika take two take one nikajisahau kama nikunywa
dawa nikanywa na kupoteza fahamu,”anasema Elly G.
Msanii huyo ambaye baada ya kunywa pombe hiyo huku akiwa ametumia
dawa aliishiwa nguvu na kutokwa na mapovu mdomoni hadi walivyoanza
kumpatia huduma ya kwanza na kuokoa maisha yake baada ya kuchanganya na
dawa mwenyewe anasema Mungu alikuwa upande wake kwani hata zilizomuokoa
ni za asili kwani kutoka sehemu waliyokuwepo hadi kufika Hospitali ni
mbali na hakuna usafiri wa haraka.
No comments:
Post a Comment