Kupitia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, Diamond amefunguka kuhusu sababu ya yeye kuchelewa kupanda stejini.
“Nililipwa pesa nusu, nikawa natakiwa
nikifika Nairobi nimaliziwe pesa yangu yote iliyobaki lakini baada ya
kufika Nairobi nikafanya show nikapewa pesa tena nusu iliyobaki
sikupewa,” amesema Diamond.
“So kufika Mombasa nikasema siwezi
kupanda kwenye stage mpaka nimaliziwe pesa yangu sio, kwasababu ilikuwa
imebaki kama dola elfu sita na kitu, saba kasoro hivi. Nikasema mpaka
nimaliziwe pesa yangu ndio nipande kwenye stage. Sababu kulikuwa na
uongo uongo kidogo, ‘ukishuka utapewa’ unajua sisi wasanii
tulishadhulumiwaga sana, mtu huwezi kumwamini kwamba upande stejini
halafu ushuke, lazima upewe chako.
Nikasema ‘mimi nataka mnilipe hela yangu
ndio nipande kwenye stage’. Halafu wakati huo show imejaa, sijawahi
kuona show iliyojaa hivyo. So baada ya kukamilishiwa pesa yangu ndio
nikatoka nikaenda stejini saa tisa hiyo na kitu. Before kabla sijafika
watu walikuwa wameshaanza kufanya vurugu, watu walipiga machupa nasikia,
vurugu kinomanoma. Lakini namshukuru mwenyezi Mungu nilipofika mimi
zile jaziba zote zikapungua watu walikuwa na mizuka.”
No comments:
Post a Comment