19 August 2013

ANGALIA PICHA ZA SHEIKH PONDA ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..Picha Zaidi Bofya Hapa  MATUKIO NA MICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname