![]() |
| Jemma Benjamin |
Yapo
matukio mengi yaliyotokea na yanaendelea kutokea katika karne ya 21
ambayo husikikitisha na yapo ya kushangaza kwa jinsi yalivyotokea,
lakini hili pia ni moja kati ya yaliyowahi kushangaza na litaendelea
kushangaza.
Wengi
tunaamini kuwa mtu hupata mshtuko baada ya kupewa taarifa mbaya ama
kushtuliwa kutokana na uoga wa kukwepa ajali. Lakini msichana Jemma
Benjamini (18) alifariki kutokana na hisia alizopata baada ya kukiss kwa
mara ya kwanza maishani mwake (First Kiss), April, 2009.
mara ya kwanza maishani mwake (First Kiss), April, 2009.
Kwa
mujibu wa mtandao wa telegraph wa Uingereza, Msichana huyo muingereza
ambae alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, alipoteza maisha baada ya
kupigwa busu na mwanafunzi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Daniel
Ross (21) nyumbani kwao na kijana huyo baada ya kutoka kwenye mtoko wa
usiku kama marafiki.
Lakini katika
mishemishe za kukaa pamoja kwa dakika kadhaa kwenye sofa
wakibadilishana maelezo kadhaa walijikuta wakikiss taratibu, muda mfupi
baada ya kiss hiyo Daniel alimuona mwenzake analegea taratibu huku macho
yake yakiishiwa nguvu na kisha kutulia kabisa.
Hali hiyo
ilianza kumtisha kijana huyo ambae anasema hawakuwahi kuwa na mahusiano
ya mapenzi kabla, na hiyo ilitokea tu wakajikuta wanakiss.
“Haikuwa
mahusiano ya mapenzi lakini tulikuwa tukikutana mara kadhaa kwa wiki,
tulikuwa tunaelekea bar kupata chakula na tukarudi nyumbani kwa kuwa
nilikuwa nimesahau credit card, tulikuwa tunaongea na tukajikuta
tunakiss.
“Tulienda
jikoni na baadae kwenye chumba cha kupumzika na Jema akakaa kwenye
sofa,nikaanza kuona macho yake yanaanza kulegea ghafla kushuka, na
mdomoni akaanza kutoa vijipovu vya mate kabla hajaanguka.”
Baada ya
hapo alimpigia simu mama yake kisha akapiga simu kuomba msaada zaidi wa
matibabu na ambulance ilifika na kumkimbiza hospital ambapo aligundulika
kuwa tayari alikuwa ameshafariki.
Ripoti ya
uchunguzi ya daktari ilionesha kuwa hakukua na sababu zozote za
kimatibabu zilizopelekea kifo chake. Na kwamba kifo cha msichana huyo
kimetokana na matatizo yanayojulikana kama Sudden Adult Syndrome (SADS),
tatizo dogo la moyo linaloaminika kuwauwa watu takribani 500 kila mwaka
nchini uingereza.

No comments:
Post a Comment