29 July 2013
"NIKIKUTA NINA VIRUSI VYA UKIMWI NI LAZIMA NIJIUE MAANA SIPO TAYARI KUCHEKWA".....BABY MADAHA
Msanii wa filamu bongo,Baby Madaha amefunguka kwamba siku akianza kuona dalili za ugonjwa wa UKIMWI ndani ya mwili wake atakunywa sumu kwa kuhofia kuchekwa na jamii.
Akiongea na mwandishi wetu,Madaha amedai kuwa kwa sasa anaamini hana ngoma maana siku zote hutumia Kinga (kondom) ili asiambikizwe gonjwa hilo japo hana uhakika asilimia zote maana hiyo ni mipango ya mungu.
"Siukatai ugonjwa huo kwa kuwa sijui ni lini naweza kuupata hasa ukizingatia kwamba mimi bado ni kijana mbichi ambaye bado nahitaji kuifurahia dunia"...Alisema Baby Madaha..
Katika mazungumzo hayo, Madaha anadai kwamba mpaka sasa hakuna mpenzi wake yeyote aliyekufa kwa Ngoma ingawa wapo waliofariki kwa maradhi ya kawaida na ajali....
"Nikijua tu nina ngoma ni lazima ninywe sumu ili kukwepa balaa la wabongo.Najitahidi kujilinda ili nisiudake mapema"..Alisema Madaha
Madaha anadai kwamba kitendo cha yeye kujiua mapema kitasaidia kuwaondolea wasiwasi wasanii wenzake ambao wataanza kujiuliza maswali mengi kuhusu watu aliowahi kutoka nao kimapenzi
"Nitawasaidia wasanii wengine ambao nimewahi changia nao mabwana.Najua wataumia sana, lakini ndo hivyo tena, hakutakuwa na jinsi.
"Sijasema nina UKIMWI,Hapana,nimesema kwamba ikitokea maana watu hawakawii kupindisha maneno"..Madaha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment