10 June 2013

MATONYA AFIKISHWA MAHAKAMA YA MWANZO MJINI SONGEA MKOANI RUVUMA KWA TUHUMA ZA UTAPELI

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYFoyK6bbmItlbuKciLRhvWAkVAq1iZIzqW5bH3SK9W-tlRkIMi0_RPRGzCpyvCLUkdDIpnytfSY2hBWaADe1_tY2sLGSuUiCdsZywJ0xl26XUfgCRu7ADEHJ9YqW8LlhCvgvWHmLQ-ABL/s1600/Matonya.jpg
Msanii huyo amekamatiliwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliyopo manispaa ya Songea mkoani ruvuma. Baada ya kuja ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya
fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipo amua ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia .

Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show ingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu ingine. 
Hatua iliyochukuliwa nikumvizia katika bus ndipo alipokamatwa , Hadi sasa yupo mahakama ya mwanzo , Taarifa zaidi zinakuijia endelea kufatilia katika mtandao wetu zitakuhijia kwani mwandishi wetu yupo eneo la tukio

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname